Burudani

Lamar, Shirko na Sheddy Clever kutayarisha nyimbo za washiriki 6 walioingia fainali ya EBSS

Watayarishaji watatu wa muziki nchini, Lamar, Shirko na Sheddy Clever watatayarisha nyimbo za washiriki 6 wa shindano la Epiq Bongo Star Search walioingia fainali.

1452502_603736013006719_1120364618_n

Washiriki hao ni Amina Chibaba, Maina Thadei, Elizabeth Mwakijambile, Melisa John, Emmanuel Msuya na Mandela Nicholas.

Katika mpango huo kila producer atatayarisha nyimbo za wasanii wawili. Lamar atafanya nyimbo za Elizabeth Mwakijambile na Melisa John, Sheddy Clever atatayarisha nyimbo za Emmanuel Msuya na Mandela Nicholas huku Shirko akipewa kazi ya kutengeneza nyimbo za Amina Chibaba, Maina Thadei.

Fainali ya shindano hilo inatarajiwa kufanyika November 30, Escape One, jijini Dar es Salaam ambapo mshindi wa kwanza ataibuka na kitita cha shilingi milioni 50 pamoja na bima ya afya ya mwaka mzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents