Burudani

Lady Jaydee: Wanawake wengi wanaishi katika ndoa zisizo na afya kwa uoga wao

Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye mahusiano mapya ya kimapenzi na Spicy wa Nigeria, muimbaji mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Lady Jaydee amedai kuwa wanawake wengi ni waoga wa kuanza maisha mapya ya mahusiano.

Jaydee ambaye aliachana na mumewe Gadner G Habash ambaye alikuwa naye takribani miaka 13, amesema watu wengi wanapokuwa kwenye mahusiano kuna maisha wanakuwa wameyatengeneza, hivyo inakuwa ngumu kuondoka na kuyaacha.

“Wanawake wengi wanashindwa kutoka kwenye mahusiano, kwenye ndoa zisizo na afya ni kutokana na wao kutojiamini. Kwanza si jambo rahisi sana kama umekaa na mtu muda mrefu harafu uamue tu kuwa unaondoka. Kuna maisha ambayo mmejenga pamoja kwa hiyo unapoondoka unakwenda kuanza maisha mapya, watu wengi lile suala la kwenda kuanza maisha mapya ndiyo huwa wanaliogopa,” Jaydee amekiambia kipindi cha Wanawake Live cha EATV.

Jide ameongeza kuwa kwa upande wake aliamua kuachana na mahusiano yake ya zamani ambayo yalidumu kwa miaka mingi na kuamua kusonga mbele kwa kuwa hayakuwa na faida kwake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents