Burudani

Lady Jaydee azitaja sifa za mwanaume amtakaye kwa sasa

Baada ya kutangaza kuwa kwa sasa yuko single, miongoni mwa maswali ambayo Lady Jaydee amekutana nayo ni kuhusu sifa za mwanaume ambaye anamtaka awe mpenzi wake kwa sasa.

JIDE2

Kupitia Instagram Jide aliorodhesha sifa za mwanaume amtakaye kwa sasa, soma huenda ukawa nazo (kama wewe ni mwanaume mwenye ndoto za kuwa na staa huyo).

Yapo maswali mengine pia ambayo yanahusiana na mahusiano ambayo ameyajibu.

SWALI: Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa?
JIBU : Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.
Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona )
Asiwe tegemezi
Hata km sio tajiri lakini asinitegemee
Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar ,
Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale
Nikikohoa tu awepo hapo

SWALI: Una boyfriend sasa hivi?
JIBU : Nashindwa kutofautisha boyfriend na lover, wanaojua kizungu wanaweza kunisaidia.
Ila kama ni kwa maana ya rafiki wa kawaida wa kiume,
Nina boyfriends not boyfriend By the way, marafiki zangu wengi ni wanaume zaidi kuliko wanawake. Kama nimeielewa kwa maana hiyo ninayodhania mimi.
Ila kama sio maana hiyo, sina boyfriend then.

SWALI: Eti una boyfriend mzungu?
JIBU : Nina marafiki wa kiume kadhaa ambao sio raia wa hapa, wenye ngozi tofauti na yangu, urafiki wetu ni wa kubadilishana mawazo, kwenda dinner, ku party kiaina na kualikana ma nyumbani kufungua Champagne na kuchoma nyama.
Kama mmeniona nao huko, we were just having fun, nothing serious.
Na sehemu nnazo kuwa nao ni kwenye mkusanyiko wa watu wenye jinsia tofauti.
Not in a bedroom.

SWALI: Una mpenzi kwa sasa?
JIBU : Ndio, ninae mpenzi kwa miaka mingi sana.
Ananipa karibia kila nnachotaka,
Amenijengea nyumba
Ameninunulia viwanja
Ameninunulia magari
Ananilisha na kunivisha
Anasomesha ndugu zangu
Amenifungulia restaurant Na ameahidi kuninunulia Beach House, na Land Rover model ya 2015.
Ila hizo ni ahadi, bado hajazitimiza.
Kila nikitaka kwenda holiday anagharamia kila kitu
Nikikohoa nataka kwenda kwa fasi ya Paris ana lipa
Tena ananilipiaga ndege business class
Sasa hivi ameniahidi kunilipia trip ya Italy nikawaone kina Kayumba….Ma shopping n.k Hajawahi kunisaliti
Jina lake anaitwa MUZIKI

Maswali yote yanahusu mapenzi / mahusiano lakini nafikiri hayahusiani na ndoa,
Hivyo swala la ndoa naomba nilitenge nitalijibu Ijumaa / Friday ndio litakuwa no. 10 na la mwisho Vipi kwani, mbona wengine mnasonya?”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents