Burudani

Lady Jaydee athibitisha ‘Rosella’ kuwepo kwenye albamu ya Woman

Tegemea kuusikia wimbo mpya wa H_Art The Band na Lady Jaydee ‘Roesella’ kwenye albamu ya Woman ambayo inatarajiwa kuachiwa Machi 31 ya mwaka huu.

Jaydee amethibitisha wimbo huo kuwepo kwenye albamu hiyo wakati akiongea kwenye kipindi cha FNL cha EATV. “This one is different. Hivi malalamiko yapo kweli? Labda Rosella lakini hakuna malalamiko zaidi,” amesema muimbaji huyo.

Jide ameongeza kuwa sherehe za kuizindua albamu hiyo zitafanyika katika viwanja vya Lugalo Golf na kiingilio kitakuwa ni shilingi 20,000 kwa sehemu ya kawaida, 50,000 upande wa Vip na 500,000 kwa meza ya watu 10.

Hii itakuwa ni albamu ya saba ya malkia huyo wa Bongo Fleva ambapo nyimbo nyingine zinazotarajiwa kusikika kwenye albamu hiyo ni pamoja na ‘Ndi Ndi Ndi’, ‘Sawa Na Wao’, ‘Together Remix’ na nyingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents