Lady Jay Dee

Lady Jaydee apata shavu la kuwa balozi wa bidhaa za kampuni ya vipodozi ya Sweden Oriflame

Kampuni ya vipodozi ya Sweden Oriflame Cosmetics imetangaza uteuzi wa wanawake watu maarufu wa Afrika Mashariki kuwa mabalozi wa bidhaa zao katika nchi zao.

Jide
Jide akiwa na viongozi wa Oriflame Afrika

Mwanamuziki Lady Jaydee amepata shavu la kuwa balozi wa bidhaa za kampuni hiyo nchini Tanzania huku mwanamuziki Juliana Kanyomozi amekuwa balozi wa bidhaa za kampuni hiyo nchini Uganda na Jamila Mbugua amekuwa balozi wa bidhaa hizo nchini Kenya.

“Lady Jaydee, Juliana and Jamila have been named because their style and approach to beauty is the ideal representation for the Oriflame brand. They are strong and talented women who many people across East Africa readily identify with,”alisema mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo Afrika Mashariki Mr. Klas Kronaas.

Mkuu wa Masoko wa kampuni hiyo Afrika Mashariki bwana Harry Njagi amesema mabalozi hao pamoja na mambo mengine, pia watakuwa wakihusishwa katika matukio ya bidhaa za kampuni hiyo kuwakilisha bidhaa za Oriflame kwa muda wa mwaka mzima.

Source: www.oriflamme.com

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents