Burudani

Lady Jay Dee azungumzia tuhuma za vyombo vya habari kuwanyonya wasanii ‘mimi kwa sasa nipo sawa’

Msanii mkongwe wa muziki nchini Lady Jay Dee amefunguka na kuzungumzia tuhuma za vyombo vya habari kuwanyonya wasanii ikiwa ni wiki moja toka amalize mgogoro wake na kituo kimoja kikubwa cha redio nchini, Clouds Media Group.
Buff Bantam Hen {Gallus gallus domesticus} with nine of her ten chicks, 2-days-old. The tenth chick is under her
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Sawa na Wao’ aliungana na wasanii wenzake wanaowania Tuzo za EATV kufichua siri ya mafanikio yao mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Kampasi ya Mlimani), huku wakiwataka wanafunzi hao kuuliza baadhi ya maswali.

Moja kati ya swali ambalo aliulizwa muimbaji huyo na mmoja kati ya wanafunzi wao, ni jinsi gani wasanii wanakabiliana na changamoto ya baadhi ya vyombo vya habari kuwanyonya wasanii wa muziki.

Katika kujibu swali hilo, Lady Jay Dee alisema sio vyombo vyote vya habari ambavyo vinawanyonya wasanii huku akiwataka wasanii pamoja na vyombo vya habari kujieleza kuhusu suala hilo.

“Kuhusiana na masuala ya vyombo vya habari kuwanyonya wasanii sina uhakika kama ni vyombo vyote vya habari ambavyo vinafanya hivyo na hapa tupo na moja kati ya vyombo vya habari labda wao watuelezee kama kuna tatizo kama hilo,” alisema Lady JayDee.

“Lakini mimi binafsi siwezi kuwa shuhuda wala kumshutumu mtu sipo hapa kwa sababu hiyo lakini maneno kama hayo yanasikika na watu wanalalamika. Lakini ni vyema kila mtu apate nafasi ya kujieleza ila mimi kwa sasa hivi nipo sawa.,” aliongeza muimbaji huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents