Burudani

Lady Gaga kutumbuiza kwenye ‘Super Bowl 51 Halftime Show’ mwakani

Msanii wa muziki wa Pop Marekani, Lady Gaga amepata shavu la kutumbuiza kwenye mapumziko (half time) ya fainali ya Super Bowl 51 mwakani.

lady-gaga

Kupitia mitandao yake ya kijamii, muimbaji huyo amethibitisha hilo kwa kuandika, “It’s not an illusion. The rumors are true. This year the SUPER BOWL goes GAGA! @nfl @FOXTV @pepsi #PERFECTILLUSION #GAGASUPERBOWL.”

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa msanii huyo kutumbuiza kwenye fainali hizo zitakazofanyika Februari 5, 2017.

Wasanii wengine waliowahi kutumbuiza kwenye fainali hizo ni pamoja na Madonna, Michael Jackson, Prince, Usher, Bruno Mars, Beyonce, Coldplay na wengine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents