Burudani

Lady Gaga achukua nafasi ya Beyonce kutumbuiza kwenye Coachella

Baada ya wiki iliyopita Beyonce kulazimika kusitisha kwenda kutumbuiza kwenye tamasha la Coachella Valley Music and Arts, mwaka huu kutokana na kuwa mjamzito Lady Gaga amedondokewa na shavu hilo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Gaga amethibitisha kutumbuiza kwenye tamasha hilo kwa kuweka cover la tangazo lake na kuandika, “Let’s party in the desert! ????✌️????.”

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika Jumamosi ya April 15 katika viwanja vya Empire Polo, Indio mjini California ambapo wasanii kama Kendrick Lamar, Radiohead, The XX, Justice, Lorde, Father John Misty, Bon Iver na wengine wanatarajiwa kutumbuiza.

Hata hivyo kuna uwezekano mkubwa Queen Bey akashiriki kwenye tamasha kama hilo la mwakani. Inadaiwa kuwa tamasha la Coachella ndio linaongoza kuingiza fedha nyingi duniani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents