Bongo5 Makala

Kwanini lawama kwa promota haziwezi kumwepusha Diamond kupoteza mashabiki

Kutofanyika kwa show ya kimataifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi wa Diamond jijini Stuttgurt, Ujerumani na kusababisha uharibifu mkubwa, kulichukuliwa na watu wengi kama ajali kazini.

diamond

Sababu za Diamond kuchelewa kupanda stejini kulikotokana na kudai alipwe fedha yake iliyokuwa imesalia kwa promota, ilikuwa ya msingi kabisa. Na pia kampuni yenyewe iliyoandaa show hiyo ilieleza kwa urefu kilichosababisha na pia kuahidi show ya bure kwa mashabiki wa Diamond.

diamond germany

Hilo lilipita na kila upande ukaganga yajayo. Ijumaa hii Diamond alikuwa afanye show nyingine jijini London, Uingereza. Bahati mbaya show hiyo ambayo yeye mwenyewe kama kawaida yake aliipigia promo sana, haikufanyika. Kama ilivyokuwa ya Ujerumani, mashabiki walimsubiri staa huyo kwa masaa kibao wasimuone akitokea. Baada ya kuonekana kunakucha bila dalili ya Diamond kupanda jukwaani, wengi walianza kudai warudishiwe fedha zao. Na kwa mujibu wa mtu aliyekuwepo kwenye show hiyo, polisi walisaidia kurejesha amani katika ukumbi huo, lasivyo yangetokea kama ya Ujerumani.

Pia anadai kuwa promota wa show hiyo alikamatwa.

“I was there brov it was maad trust me, even police got involved with that shit, they had to calm people down until seven in the morning, people wanted their money back he I’ll pay the price cause he got arrested,” ameandika.

Diamond amemtupia lawama promota huyo ambaye si mara ya kwanza kufanya naye kazi na kumuita tapeli.

“Tafadhari ndugu zangu wa UK!!!….kuweni makini sana na promoter huyu (Victor – Dj rule) mnaposikia kaandaa show, party au Hafla yoyote…ni vyema kuziepuka na kutohudhuria kabisa kwasababu ni tapeli…. si unajua aisifiae mvua imemnyeshea… basi mie nimeloa kabisa.”

Pamoja na kwamba Diamond hana makosa katika hili, hawezi kukweka lawama kutoka kwa mashabiki wake walio na kinyongo naye. Shabiki hatotaka kujua makubaliano kati ya msanii na promota. Anachojua yeye ni kuwa show ilitangazwa kuwa itafanyika na yeye akanunua tiketi kuja kushuhudia.

Si kazi yake kutaka kujua kama msanii amelipwa fedha yake ama lah! Kama Diamond alikuwa anamfahamu vyema DJ Rule kuwa si mwaminifu, kwanini alikubali kufanya naye show? Sijui makubaliano yao yalikuwa vipi, lakini kwanini alikubali kulipwa fedha nusu kabla ya kutumbuiza?
Ni yaleyale kama ya Ujerumani.

Wengi tunamchukulia Diamond kama mfano wa msanii wa Tanzania aliyefanikiwa na tunategemea kuwa makubaliano yake yanapaswa kuwa kwamba promota anatakiwa kumlipa ama fedha nusu, robo tatu au fedha yake yote (kama anamuamini) na kusaini mkataba unaowafunga wote. Mara nyingi mikataba husema fedha iliyosalia inatakiwa imfikie msanii wiki moja ama siku chache kabla ya show. Wengine hukubaliana fedha hiyo alipwe msanii pindi anapowasili katika mji huo ama anapofika hoteli.

Ninafamu kuwa Diamond na timu yake wako smart mara nyingi lakini nashindwa kupata jibu la kwanini makosa kama haya yanaendelea kutokea tena katika show za kimataifa. Kuna uwezekano mkubwa kama hajapoteza mashabiki wengi, basi heshima waliyokuwa nayo kwake imepungua.

Yeye na timu yake wanapaswa kuwa smart na kusaini mikataba ya show isiyokuwa na ahadi za kupeana fedha iliyobaki siku ya show. Promota wanapaswa kujipanga na wanapotafutwa na promota wenye longolongo wasiwe na aibu kuwakatalia moja kwa moja kutunza heshima yao.

Matukio kama haya yanaweza kuwa mabaya kwa biashara pia kwakuwa baadhi ya promota wa kimataifa hawapendi kufanya kazi na wasanii wenye CV mbaya katika show zao zilizopita.

Haya ni baadhi ya maoni ya watu mbalimbali yanayofanana kiasi na ya kwangu.

kiswigogodfrey

Play back concert 2 times inabuma hiyo ni kukosa management imara yenye kusimamia mikataba yako. Umetoka bongo hadi UK bila kujua mikataba yako. Hilo fans wako haliwahusu wao ni burudani ndio haki yao hayo mengine utajijua na promota wako. Na kama jamaa amekupiga kama ulivyo post ni vzr ukafuata taratibu za kisheria ndio zitoe hukumu na ukishinda ndio umwanike kwenye social network.Kama hujafanya hivyo tegemea kesi ya madai kutoka kwa mshikaji ingawa umeshapata hasara kwa kukosa umakini na management yako, it’s over.

jamal_huwel

Men mara ya pili hii hebu badilisha system ya mikataba yako. Pokea angalau 60% of the cash kabla ya shoo. Watakuharibia mtaalamu wetu tutakosa talent yako tena

Allykikasha

PLZ PLZ PLZ READ THIS….DIAMOND wewe ushakuwa msaani wa kimataifa na watu nao wanakufahamu,, jaribu kutafuta timu ya uhakika mtu anayejua ishu ya marketing professionally,, uwe na mwanasheri hata yule wa kumlipa tu pale unapoingia mkataba,, achana na waki BABU TALE wao umeneja wao ni wa show za mikoani tuu,, then hana creativity yoyote zaidi ya kuwanufaisha,, jaribu now to change,, uwe na watu wenye uwelewa na kitu unachokifanya,, Germany imetokea ,, then BAB TALE anasema eti imesaidia kukutangaza,, very stupid comment then ISSUE SIO PROMOTERS ITAFIKIA SIKU FANS NOW WATAONA KILA SHOWS ZAKO NI ZA KITAPELI ,, PEOPLE THEY CHANGE.

carryandy

Acha kuwatangazia mashabiki wako show kabla hujalipwa hela kamili, vinginevyo unajiharibia biashara 2nd time hii, hujajifunza tuu? Na sijui kama unakuwa na makubaliano ya maandishi kabla hujajiingiza kuwambia fans wako utkuwa somewhere. , jipange utaja pata matatizo makubwa nchi za watu hizo oh!

rayna_rayna_

Mmmhh um not sure kama anaweza kukufanyia ivyo maybe umeenda bila contract ndo mana imetkea yote..next tym jipange na team yko najua jamaa ni mtu mkubwa and also unaweza kwenda mshitaki ubalozini kwa kukupotezea mda na kukupotezea issue maybe it will help

callyrissanen

Pia kuwa makini chibu. Hao police wa nchi za wenzetu wakifanya mawasiliano unaweza hata huko germany ushindwe kufanya show. Tafuta mwanasheria wa hiyo mikataba yako. Na uwe unamaliziwa kulipwa pesa za show unapofika tuu kwenye nchi husika, msisubiri hadi muda wa onyesho ndio muanze kudaiana. Inakuwa rahisi kutoa tamko kwa mashabiki mapema kama hutohudhuria mapema iwezekanavyo ili wasisumbuke

irymamur_de_star

Inaonekana management yako haipo makini kabisa kwan inatokea nn?? hadi mtu anakutapeli cc mashabiki zako tunaumia xana kuckia ivyo na maswal mengi juu ya hilo kwan thamani yako ya show za nje inapungua xaxa kuwa makini na hao bakoharam sio watu wazuri kwako na huyu jamaa xaxa mi sioni kazi yake @babutale mi nakupa pole xana kwailo!!!! ila hujafafanua vzur juu ya hilo tujue ilikuaje yani tujue mwanzo mwisho kwa maelezo kwan tunahaki kama mashabiki zako pendwa!!!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents