Diamond Platnumz

Kwanini Diamond Platnumz alilia kwenye video hii?

Hakuna siri kuwa Diamond Platnumz na Yemi Alade walifanya kazi nzuri kwenye msimu wa pili wa Coke Studio Africa. Miongoni mwa nyimbo zilizofurahiwa zaidi ni Johny ya Yemi na Ukimwona ya Diamond ambazo waliziimba pamoja.

https://www.youtube.com/watch?v=fbsrzW_fKyo

Lakini kilichofurahisha zaidi na pengine ambacho watu wengi hawajakigundua ni pale Diamond alikuwa akijadiliana na producer wa video ya live performance ya ‘Ukimwona’ ambapo alikuwa akimweleza idea mbalimbali za kuifanya vizuri zaidi.

Hata hivyo kwenye maongezi hayo Diamond alijikuta akibubujikwa na machozi kwa kukumbuka kitu cha huzuni kwake.

“This background is taking me to another world I am telling you,” Diamond alimwambia producer huyo. “It reminds me of those days,” anaongeza Diamond huku akiinama kuficha macho yake. “It’s a very powerful song,” anasema producer.

“Are you okay,” producer anauliza na Diamond kusema yuko sawa ilhali akiendelea kuinama.

Swali ni kitu gani alichokikumbuka hadi kumfanya atoke machozi? Ni suala kuhusu mapenzi au maisha? Tutamuuliza tukipata nafasi!

Mashairi ya Ukimwona yalimkosha pia Yemi Alade ambaye alisema wimbo huo una ‘content’ ya hatari kitu ambacho wasanii wengi hawaandiki. Tazama video hiyo utaipenda.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents