Bongo5 Makala

Kwani ni Lazima uvae ki’kike’ ili Uchekeshe?


Siku hizi ukitaka kuwa mchekeshaji (mwanaume) hata kama huna kipaji hicho kuna njia moja maarufu sana unayoweza kuifanya. Nenda kanunue weaving, jipake lipstick na wanja, bandika kope, nunua machungwa mawili ili utengeneze matiti, tafuta nguo utengenezee makalio makubwa nyuma, aaah! tayari umeshahitimu chuo! Umeshakuwa mchekeshaji tayari.
Rahisi sana sio? Ndo vichekesho maarufu vya Tanzania hivyo. Na cha kufurahisha zaidi ni kuwa wanawake wengi tu wanapenda vichekesho vya aina hiyo.” Kwangu naona haina shida kwa vile wanaigiza tu na ujumbe unafika kwa jamii iliyokusudiwa na tunaburudika, anasema dada mmoja aitwaye Conchesta baada ya kumuuliza anavionaje vichekesho hivyo.
Kwa upande wake msichana aitwaye Minza Razack anasema,”to my side naona wanafanya vile ili wafikishe ujumbe kwa hadhira waliyokusudia,kwa mfano, mwanaume hawezi kuigiza kama shoga afu avae kidume tu.”
Wengine lakini wana mtazamo tofauti kama asemavyo Julieth Hubert, “Kiukweli mi sipendi, ila kama ndo kunamfanya apate riziki basi hakuna jinsi. Ni vile naona huwa wanalazimika kufanya hivyo. Nadhani hata wao hawapendi kufanya hivyo toka moyoni ila kwakuwa ndo sababu inayoleta uhalisia wa kitu inawabidi. Kiukweli siwezi kumshauri kufanya hivyo.”
“Kawaida tu ila wakijiremba sana wanaboa , kama ni my boy kwa kweli I won’t allow it,” alisema dada mwingine aitwaye Magreth.
Amanda Krauss ni mwandishi na mchambuzi wa masuala mbalimbali kwenye mtandao nchini Marekani anauzungumziaje uchekeshaji huu wa kuigiliza wanawake:
“Huenda mimi ni mtu pekee duniani ambaye huwa sioni kama vinachekesha. Naviona vinaboa na vinatabirika na hukera pia.
Pamoja na kwamba vichekesho vya aina hii vina umaarufu mkubwa nchini kiasi ambacho makundi mawili hasimu ya The Comedy ya EATV na Original Comedy ya TBC huitumia njia hii kama silaha yao katika uchekeshaji, mtazamo wa watu wengi wanaoangalia comedy za nje ni kuwa watu hawa wameishiwa ubunifu.
Wachekeshaji maarufu wa vichekesho vya kusimama (stand-up) kama Kelvin Hurt, Chris Rock, Steve Harvey na wengine hawahitaji kushona weaving na kujipaka lipstick ili wachekeshe maelfu ya watazamaji waliolipa kiingilio kwenda kuwaangalia.
Tena hawa wana kazi kubwa zaidi kwakuwa wanachokizungumza ndicho kinachosikika moja kwa moja bila kuwa na muda wa kutoa makosa. Pamoja na ugumu wa stand-up comedy hakuna hata siku moja watu hawa huvaa nguo za kike ili watu wacheke.
Ludovick Peters wa Tabora anasema, “it’s because they don’t know the characteristics of a drama. Yes, it’s true that a comedy, is meant to make people laugh and be amused, but not to the extent of donning feminine attire. Had you ever seen Mr Bean in a female gown?”
Kwa mfano huo wa Mr Bien mmoja wa wachekeshaji maarufu sana duniania utagundua kuwa ni maneno, vitendo na story wanazotoa wachekeshaji wazuri ndivyo vinavyowavunja mbavu watu.
Kwani ni nani aliyesema wanawake hawachekeshi? Kuna raha yake pia kumpata mhusika halisi sehemu inayohitaji mwanamke na sio kutumia midume yenye miguu yenye manyoya na iliyokomaa kama jiwe.
Wanawake wengine wanaviona vichekesho hivyo kama jukwaa la kuwadhalilisha kwakuwa hakuna mwanamke anayejiremba kama wao wafanyavyo kiasi cha kuwafanya waonekane kama nyani aliyepakwa make-up.
Hebu jiulize kwanini kipindi cha vichekesho cha ITV cha Mizengwe cha akina ‘Wa Ukae’ bado kinapendwa pamoja na kuanza muda mrefu sana enzi za marehemu Max na mchekeshaji aliyegeuka mtangazaji, Zembwela bado kinapendwa hadi leo na hakijawahi kuchuja.
Mwanamke pekee waliyenaye kwenye vichekesho hivyo ambaye tunathubutu kusema anaweza kuwa among of the funniest women in Tanzania, anawakilisha vizuri na ujumbe unafika kwa uhalisia wake.
Hauhitaji kuvaa kike ili kuchekesha, unahitaji kuchekesha kwa namna unavyoyaweka maneno yako. Mpoki anasifika sana kwa kutumia maneno yake tu kuchekesha. Kwenye tuzo za Kili mwaka huu wahudhuriaji walikuwa wakiangua vicheko kama wendawazimu kutoka kwa Mpoki aliyekuwa amevaa suti tu.
Kuna haja ya wachekeshaji nchini kuja na ubunifu mwingine wa uchekeshaji kwa kutumia mambo halisi yanayotokea kwenye jamii ya kitanzania kama wafanyavyo mizengwe.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents