Kama sio DStv potezea
TECNO Spark 2

Burudani

Kwa msanii mwanamke ni stress sio kiki – Ray Vanny

By  | 

Kwa muda mrefu wasanii wamekuwa wakituhumiwa kuwatumia wanawake hususan wenye majina makubwa kama njia ya kutafuta kiki ili majina yao yaendelee kuwa mdomoni mwa mashabiki.

Hali hiyo imesababisha kutokuwepo na imani kuhusiana na ukweli katika mahusiano mengi ya mastaa wa Bongo ambapo wengi huhusishwa na kutafuta kiki.

Hata hivyo Ray Vanny amedai kuwa kwa msanii, mwanamke sio kiki bali ni stress tu. Akizungumza na Dizzim Online Jumanne hii, Ray alidai kuwa wanawake wamekuwa wakiwapa zaidi stress wasanii na wengi wakijikuta wakipotea kabisa.

Alidai kuwa uhusiano hasa pale unapoanza kuingia kwenye migogoro humfanya msanii apoteze concentration kwenye muziki wake na kupoteza vingi.

Alitolea mfano hata habari za udaku kuhusu girlfriend wa staa fulani kuhusishwa kuwa na uhusiano na mtu mwingine huwachanganya wasanii sababu huonekana kama wana udhaifu.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments

Bongo5

FREE
VIEW