Habari

Kuwa Mwaafrika nchini India: Tunaonekana kama mashetani

Mwaka mmoja wa masomo nchini India umekuwa mgumu kwa  Zaharaddeen Muhammed, 27. Anasoma shahada ya pili kemia kwenye chuo kikuu cha Noida International [University]. Kwa ni nchini Nigeria.

image

Anasema watu wa huko humuona tofauti na asiyeweza kuaminiwa. “Ninaongea kihindi na mara nyingi hucheka. Lakini ninapowapa watoto wa majirani biskuti, hawakubali,” alisema kwenye kongamano la Africa-India Solidarity huko New Delhi.

Anasema baada ya mwaka mmoja, ndoto yake kubwa bado hajaitimiza: kualikwa kwenye harusi ya Kihindi. “Sijawahi kwenda nyumbani kwa mhindi yeyote kama rafiki. Hakuna aliyewahi kunitembelea,” anasema Zaharaddeen.

Mapema mwaka huu, mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania alipigwa na kuvuliwa nguo hadharani huko Bangalore na kundi la watu wenye hasira waliokuwa wanalipiza kisasi cha ajali iliyosababishwa na mwanafunzi wa Somalia asiyemjua kabisa.

image

Zaharaddeen aliongelea tukio hilo la Bangalore: “Alikuwa akitembea tu hapo [mwanafunzi wa Tanzania]. Ingeweza kutokea kwa mtu yeyote kati yetu.”

Hata kupata vyumba vya kupanga wakati mwingine huwa mtihani kwa watu weusi nchini India.

Rohtas, dalali wa nyumba anasema huambiwa na wamiliki wa nyumba kuwa asiwaoneshe watu weusi sababu huaminiwa kuwa wanafanya biashara za madawa ya kulevya na shughuli zingine za kihalifu.

Mwanafunzi mmoja wa kike alidai kuwa si wenye nyumba tu wenye imani hiyo: “Wauzaji wa maduka huangalia fedha ninazowapa kuhakikisha kama sio feki,” anasema.

“Ni dharau na si haki. Sisi ni watu wenye furaha na wachangamfu. Lakini India tunajikuta tukiwa na hasira tu.”

Kwa upande wa Ibrahim Djiji Adam, 25 mwanafunzi wa biashara kutoka Libya anasema: Mara nyingi tunaonekana kama mashetani, wauza unga au changudoa.”

Chanzo: Al Jazeera

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents