Burudani

Kuongelewa vibaya kunazidi kulikuza jina langu – Harmorapa

Rapper ambaye kwa sasa ana kiki kubwa Bongo, Harmorapa amezungumzia madai kwamba anabebwa na wimbi la kiki wala hayupo kwenye game kudumu.

Hakijatosha, Harmorapa alipata nafasi pia kuzungumzia ishu ya wanaomuongelea vibaya na hata kumtukana. Nilipata nafasi ya kupiga stori na Harmo na alikuwa na la kuwaambia wanaomsema vibaya. “Watu ambao wanahisi Harmorapa hatodumu kwenye game kwanza wanakosea halafu pia naweza nikasema kwamba wanamkufuru Mungu kwa sababu Mungu ndiye anayepanga na kupangua,” alisema rapper huyo.

Aliendelea kusema…”Kama mimi binafsi nimejipanga sana vya kutosha. Unajua kwamba maneno yao mimi hayanivinjii chochote ni ile sawa na kumpiga chura teke na kumwongezea mwendo. Wanavyoniongea mimi ndo wananipa power na wananipa maujuzi na wananipa kuweza. Ni wao wananiweza mimi kuweza na kukaza ilmradi niweze kufanya kazi nzuri.”

Katika hatua nyingine nilitaka kujua iwapo Harmonize amemjua kabla awe supa staa au vipi. Alinijibu kwa kusema kwamba hakuwa akimfahamu muimbaji huyo kutoka WCB kabla hajakuwa staa. Wakati akiendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘Kiboko ya Mabishoo’, Harmorapa amewaahidi mashabiki wake makubwa mwaka huu na amewataka wawe tayari kushuhudia maangamizi atakayofanya kwenye game mwaka huu.

Na: Teddyza Agwa
Instagram @teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents