Habari

Kundi la majizi liitwalo `kapu bovu` laibuka Mwananyamala

Kundi hatari la wezi linalotumia bastola na mapanga, limeibuka na sasa linawapeleka puta wananchi wa eneo la Mwananyamala na maeneo jirani ya Magomeni, Tandale, Kijitonyama, Mburahati na Kinondoni.

Na Adam Fungamwango, Mwananyamala

 
Kundi hatari la wezi linalotumia bastola na mapanga, limeibuka na sasa linawapeleka puta wananchi wa eneo la Mwananyamala na maeneo jirani ya Magomeni, Tandale, Kijitonyama, Mburahati na Kinondoni.

 

Kundi hilo lenye watu wapatao 15 linalojiita `kapu bovu` inadaiwa kazi yake ni kuvamia bar, kumbi mbalimbali za starehe, majumbani na hata njiani na kuliza watu kila walichonacho.

 

Askari wa kituo cha polisi cha Mwinjuma wamethibitisha kuwepo kwa kundi hilo. Kadhalika askari wa sungusungu ambao hawakutaka majina yao yachapishwe gazetini wamesema kundi hilo lipo na ni tishio kwa wananchi na mali zao.

 

Imedaiwa kuwa kundi hilo hatari la `kapu bovu` linaongozwa na mtu anayejiita `Mark Sirengo` ambaye pia inaaminika anamiliki silaha ambayo hufanyiwa uhalifu.

 

Askari huyo amesema kundi hilo linaundwa na vijana kutoka Mwanyamala, Magomeni eneo la Day Break na Tandale.

 

“Wakiingia kwenye bar na sehemu nyingine za starehe wanaambia watu walale chini… wana kapu lao kubwa ambalo mateka huambiwa watumbukize kila walichonacho humo,“ amesema mmoja wa sungusungu.

 

Hata hivyo amesema kuwa hata pale ambapo watu hutii agizo la majizi hayo na kusalimisha mali zao kwenye kapu, bado hujeruhiwa na kupigwa.

 

“Wengi wana mapanga ila huwa mmoja wao ana silaha ya bastola ambayo ni mali ya huyo kiongozi wao Sirengo,“ amedai askari huyo wa kituo cha Mwinjuma.

 

Source: Alasiri

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents