Burudani

Kuna watu wanaongea, wamekasirika mimi kumsaidia Wema Sepetu – Albert Msando

Mwanasheria wa Wema Sepetu, Albert Msando amefunguka kwa kudai kuwa kuna watu hawakupenda yeye kumsaidia kisheria muigizaji huyo wa filamu ambaye hivi karibuni alishikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake pamoja na makosa mengine.

Muigizaji huyo alifika kituoni hapo February 3 na kushikiliwa na jeshi hilo kwa siku 6 baada ya jina lake kutajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuwa ni mmoja kati ya watu wanaotuhumiwa kutumia Madawa ya kulevya.

Mwanasheria huyo aliamua kumsaidia kisheria muigizaji huyo pamoja na wenzake na February 9 malkia huyo wa filamu alipata dhamana.

Baada ya tukio hilo mwanasheria huyo amedai kuna watu hawakupenda yeye kumsaidia malkia huyo wa filamu.

“Have you ever had a sister who is the opposite of you? A friend who you can not explain why he or she is your friend? I have. Having a one-on-one with Wemasepetu. Kuna watu wameongea walichoongea. Wamekasirika kumsaidia Wema,” aliandika mwanasheria huyo Instagram.

“Ila ukweli unabaki kwamba Wemasepetu has her following. I must say yeye kama ilivyo mimi na wewe sio mkamilifu. She has her share of mistakes. And failures. But she is not a bad person. She has a special heart. Her charge is “to be found in possession of small amount of narcotics drugs commonly known as bhangi. 1.85gms” nothing serious. Kweli au si kweli ni kazi ya Mahakama. Kwa hiyo kwa wale ambao wameamua kupigana vita kwa kuniattack I am leaving it to them. For me all I have to do is, guide her to being better and realising her full potential. Thats not law. Thats friendship. #PresumptionOfInnocence #EqualityBeforeTheLaw #SayNoToDrugs #TheDon #WemaWaNyumbani #Now #OneToOne #Laughing #SheIsOkay #SheIsfine #Lessons.

Muigizaji huyo anatakiwa kurudi mahakamani February 28 ili kujibu mashta matatu ambayo yanamkabili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents