Habari

Kuna simu nyingi juu ya ripoti, nawaomba tutulie kamati wanamalizia kazi yao – Waziri Nape

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amewataka wananchi kutulia kusubiria ripoti ya uchunguzi juu ya tukio la Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kuvamia kituo cha redio cha Clouds FM usiku akiwa na askari wenye bunduki.

Waziri huyo Jumatatu hii wakati akizungumza na waandishi wa habari akiwa katika kituo cha Clouds FM, alisema ameunda kamati ya watu tano kuchunguza tukio hilo huku akiahidi kamati hiyo kutoa taarifa ya tukio hilo Jumanne hii.

Jumanne hii waziri huyo ametoa taarifa kueleza nini kinaendelea kuhusu ripoti hiyo.

“Kuna simu nyingi juu ya ripoti. Nawaomba tutulie Kamati wanamalizia kazi yao, ikikamilika tutataarifiwa muda na mahali nitakapokabidhiwa,” alitweet waziri Nape Jumanne hii.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents