BurudaniVideos

Kuna mkali, mpole na mtu wa makavu: Ray Vanny aeleza tofauti za Babutale, Sallam na Said Fella katika kazi

WCB ni label yenye mameneja wengi. Maarufu zaidi ni Babutale na Sallam huku pia Said Fella akiwa mmoja wao japo yeye huonekana zaidi katika kazi za Mkubwa Na Wanawe na TMK Wanaume Family.

Mameneja hao wanatofautana vipi tabia zao katika kazi? Ray Vanny anawaelezea vizuri. “Hapo kila mmoja ana uzuri wake na ubaya wake,” Ray alisema kwenye interview na Dizzim Online.

“Bosi Sallam ni mtu ambaye anafokafoka lakini vitu vyake anakufanyia on point. Bosi Tale ni mtu ambaye anakupa favour ya vitu lakini maneno yake naye makali, hakufokei ila akikuambia unaenda kufikiria mwenyewe nyumbani, ni mtu ambaye anakupa kama ushauri,” ameongeza Ray.

“Mkubwa yeye ni mtu anayekuwaga kama hana ufagio yaani, kama mtu wa mikausho, nyimbo mbaya anakuambia hii mbaya, ‘hii hapana’ so wote naenjoy kufanya sababu wote ni mabosi wangu.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents