Burudani

Kukosekana kwa umoja wa wasanii kunasababisha wajanja wachache kunufaika – Nikki Wa Pili

Rapper wa Weusi, Nikki Wa Pili amesema kuwa kukosekana kwa umoja wa wasanii kunasababisha mambo yao mengi kuzorota.

Nikki wa Pili

Akiongea na Planet Bongo ya EA Radio, Nikki amesema ni lazima wasanii watambue umuhimu wa kutengeneza umoja wao utakaowasimamia na kuwasemea.

“Umoja ni kitu cha msingi, kwa sababu bila umoja mambo mengi ya wasanii yatazorota, na kutokuwepo kwa umoja kutatengeneza matundu ambayo wajanja wachache watapitisha mikono yao kwenye hayo matundu na watafaidika nayo, kwa hiyo lazima kuwe na umoja wa wasanii, ambapo utasimama na kuwasemea wasanii”.

Nikki aliendelea;

“Wasanii wengi pia hawaoni umuhimu wa umoja, kwa hiyo wamekosa msukumo wa kuwa na umoja, na pia chama na chenyewe kimekuwa kimezidiwa sana na kutokuwepo kwa umoja wa wasanii, kwa hiyo kimejikuta nguvu zake zimekuwa chache, lakini umoja ni kitu cha msingi sana, kuna mifano mingi kama wasanii tulivyo ungana tukatoa sauti zetu kwenye katiba tukaona matokeo yake, kwa hiyo mambo mengi ya wasanii yataweza kurekebishwa kukiwa kuna umoja”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents