AwardsBurudani

Kuchaguliwa Kili Awards kwangu ni Ushindi

“Ni mara yangu ya kwanza kuchaguliwa katika tuzo za kilimanjaro jambo ambalo limenifariji sana kwani sidhani kama nimekuwa kwenye gemu kwa muda mrefu lakini….

lamar_1.jpg

 

Kuchaguliwa kwangu ni Ushindi-Lamar “Ni mara yangu ya kwanza kuchaguliwa katika tuzo za kilimanjaro jambo ambalo limenifariji sana kwani sidhani kama nimekuwa kwenye gemu kwa muda mrefu lakini jitihada zangu za muda mfupi zimenionesha kuwa ni kiasi gani jamii imenikubali na kukithamini kile ninachokifanya”

Ni maneno yake Prodyuza mdogo kabisa anayejulikana kwa jina la Lamar ambaye ni prodyuza mdogo kuliko maprodyuza woooote wa muziki hasa wa kizazi kipya, ambapoa alianza kama utani na hata yeye mwenyewe hakutarajia kabisa kama ipo siku atachaguliwa katika kinyang’anyiro cha kili awards.

Hapo awali alikuwa akifanya kazi chini ya usimamizi wake prodyuza majani wa bongo Records na baadae akajikita katika studio za 41 Records kabla hajafungua studio yake ambayo iko maeneo ya kariakoo ijulikanayo kwa jina la fish crab.

“Ukweli kabisa nastahili kuchukua tuzo hizi kulingana na watu ambao nimepangwa nao katika kipengele cha prodyuza bora, hata kama sitabahatika kuichukua pia haitaniumiza sana kwani itakuwa imenipa changamoto kwa kiasi kikubwa sana” Aliendelea kusema Lamar

“hata kama itatokea nitaikosa hiyo tuzo kwa kweli haitaniathiri kabisa zaidi ya kunipa changamoto ya kufanya vizuri mwakani kwenye tuzo nyingine…pia naamini daima mwanzo huwa ni mgumu kwa kitendo cha kuchaguliwa tu kwangu pia yaweza kuwa ni ushindi kwangu” – Lamar.

Lama amekuwa akitengeneza mikono kibao ambayo inafanya vizuri sana kwenye medani nzima ya muziki wa kizazi kipya ikiwe ngoma ya sikuhitaji ya Keisha, Nenda ya 3D, Bounce ya Fan a mingine kibao ambayo imebamba ile mbya kwenye medani ya muziki wa kizazi kipya.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents