Burudani

KR Mullah asema hajaondoka TMK Family, aeleza amefuata nini Rada Entertainment ya TID

Rappa KR Mullah amesema yeye bado ni msanii wa TMK Wanaume Family na Radar Entertainment yupo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali kutoka kwa vijana.
KR akiwa na TID

Akiongeza na Bongo5 Jumapili hii, KR amesema hawezi kuondoka TKM Wanaume Family kwa kuwa yeye ni mmoja kati ya waanzilishi wa kundi hilo lenye maskani yake Temeke jijini Dar es salaam.

“Mimi sijaondoa Wanaume Family, bado nipo kule sema lazima ujichanganye kidogo na wasanii ili kubadili ladha ya muziki, Rada kuna vijana wengi wapya na kukaa nao kunanipa vitu fulani ambavyo vinaweza kuboresha muziki wangu,” alisema KR.

Pia KR alisema yeye ni mmoja kati ya waanzilishi wa Kundi la TMK Wanaume Family hivyo hawezi kulitosa kundi hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents