Habari

Korea Kaskazini yatishia kuishambulia ikulu ya Marekani kufuatia shutuma za udukuzi

Kwa mujibu wa Korea Kaskazini, Rais Barack Obama amekurupuka kusambaza uongo kuwa nchi hiyo ilishiriki kufanya shambulio la mtandaoni ndani ya mifumo ya kampuni ya Sony Pictures.

Pyongyang, DPRK. 9th December, 2014. Photo provided by Korean Central News Agency (KCNA) on Dec. 9, 2014 shows top leader of the Democratic People's Republic of Korea (DPRK) Kim Jong Un (front) applauding in front of the participants in the Second Meeting

Pia imeonya kuishambulia ikulu, Pentagon na Marekani yote.

Marekani inaishutumu Korea kuhusika kwenye udukuzi huo ulioifanya Sony isitishe kufanya uzinduzi wa filamu yake, The Interview inayoongelea kuuawa kwa kiongozi wake, Kim Jong-un.Jeshi la Korea Kusini limeonya kuwa lipo tayari kutumia njia zote za kivita dhidi ya Marekani.

Korea Kaskazini imesema inafahamu jinsi ya kuthibitisha kuwa haihusiki na udukuzi huo na imependekeza uchunguzi wa pamoja na Marekani. Nchi hizo ziliwahi kuingia vitani mwaka 1950-53 kwenye vita vya Korea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents