Burudani

Kolabo na Mafikizolo? Shetta azungumzia matokeo ya ‘Kerewa’

Rapper Shetta amezungumzia matokeo ya video ya wimbo wake ‘Kerewa’ na kudai kuwa yupo mbioni kufanya ngoma na wasanii wa Afrika Kusini

Shetta

Shetta ameiambia Bongo5 kuwa tayari kuna kampuni inayofanya kazi ya kumtafutia kolabo mpya nchini humo.

“Kutokana na wimbo wa Kerewa unaonyesha utanipa deal kubwa na kolabo. Kerewa unapigwa Nigeria na sehemu mbalimbali. Unajua ikifika Nigeria uongo mbaya unaweza ukapata kolabo baada ya kujulikana. Kuna kampuni niliingia nayo mkataba kule South Africa na kuna wasanii kadhaa wamewasikilizisha nyimbo zangu, wakaongea na Djs pia wakahitaji Biography yangu. Wamezungumza na Mafikizolo kwahiyo lolote linaweza likatokea. Pia wadau na wapenzi wa muziki wangu wa bongo wasubiri kidogo kwa sababu muziki wa mbele ni tofauti na wa hapa nikifanya hiyo kolabo ndipo nitakapoachia na wimbo wa hapa nyumbani, kazi zipo nyingi tusubirie tu wakati ukifika,” amesema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents