Burudani

Koffi Olomide anyimwa dhamana, aendelea kusota jela

Juhudi za wanasheria wa Koffi Olomide kutaka apewe dhamana zimegonga mwamba Ijumaa hii.

Olomide

Kesi yake ilisikilizwa leo huko Kinshasa. Anashikiliwa kwenye gereza la Makala.

“Ni aibu. Ni lazima afurahie haki zake. Mahakama zetu zina kasoro kwa makosa yaliyofanyika nje ya nchi, hasa kwenye kesi hii. Koffi anajua ukubwa wa matendo yake na aliomba msamaha. Ataendelea kukaa ndani kwa walau siku 15,” alisema mwanasheria wa mwanamuziki huyo, Master Lukoo Ruffin.

Staa huyo wa muziki wa Lingala alijikuta matatani baada ya kumpiga teke dancer wake wakati wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Ijumaa iliyopita.

Polisi wa Kenya walimkamata usiku huo na kumrudisha kwao Kinshasa hali iliyopelekea kuvunjika kwa show aliyokuwa amepanga kufanya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents