Burudani

Koffi Olomide akamatwa na polisi DR Congo

Msanii wa muziki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amekamatwa akiwa nyumbani kwake mjini Kinshasa.
230716052439

Mwandishi wa BBC Poly Muzalia anasema mwanamuziki huyo amekamatwa kwa agizo la ofisi ya mwendesha mashtaka.

Muimbaji huyo alitimuliwa kutoka nchini Kenya baada ya video kuonekana kuonesha akimpiga teke mchezaji ngoma wa kike katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema asubuhi baada yake kuwasili.

Alipangiwa kutumbuiza mashabiki wake Bomas of Kenya siku ya Jumamosi lakini tamasha hiyo ikaahirishwa.

Alikamatwa Ijumaa usiku na maafisa wa polisi wa Kenya na siku iliyofuata asubuhi akaingizwa kwenye ndege na kurejeshwa Kinshasa.

Hapo jana shirika la kutetea haki za binadamu nchini Jamuhuri ya Kimemokrasia ya Congo, liitwalo Asvoko, limeiomba serikali ya nchi hiyo kumfungulia mashataka mwanamuziki Koffi Olomide.

Source: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents