Michezo

Kocha wa Swansea City Michael Laudrup atimuliwa

Swansea City imemfuta kazi kocha wake Michael Laudrup na kumpa nahodha wa timu hiyo Garry Monk kuiongoza katika mechi ya ligi dhidi ya wapinzani wake Cardiff City Jumamosi ijayo.

Laudrup wakati yupo

Taarifa hizo zimekuja siku moja tu baada ya mwenyekiti wa klabu hiyo Jenkins kupuuzilia mbali tetesi kuwa walikuwa wamezungumzia mustakabali wa Laudrup. Uvumi ulikuwa umesambaa kuhusu hatma ya Laudrup baada ya Swansea kushindwa kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham Jumamosi iliyopita.

Hiyo ilikuwa mara ya sita timu hiyo kupoteza katika mechi nane za Ligii kuu ya Uingereza na kuiacha na alama mbili tu juu ya timu ambazo zitateremshwa katika ligii hiyo.

Monk alikuwa amepigiwa debe kuchukua nafasi hiyo ikiwa mojawapo ya njia za kuboresha kikosi hicho.

Source:BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents