Burudani

Kleyah adai wimbo wa ‘African Drum’ umempatia collabo na wasanii wa nje

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Kleyah amesema wimbo wa ‘African Drum’ ndiyo umempatia connection ya kupata collabo na wasanii wa nje akiwemo msanii bora wa kike kutoka Namibia, Chikune.

a2e4786124815cde782b596fea3534ae-1

Akiongea na Bongo5, Kleyah amesema kuwa anatarajia kufanya collabo na top female wa Namibia pamoja na wasanii wengine wa nje.

“Nina mipango ya kufanya collabo na msanii mmoja kutoka Namibia. Yeye ndiyo top female wa Namibia, Chikune,” alisema Kleyah.

“Aliipenda video ya ‘African Drum’ then tukaongea pamoja na tukaamua kufanya collabo ya Afropop. Mungu akipenda tutamaliza mwaka ujao,” aliongeza.

Kleyah ameachia wimbo wake mpya hivi karibuni ‘Sioni’ unaendelea kufanya vizuri kwenye Radio.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents