Michezo

Kipre Tchetche arudi Oman kupigania uhamisho wake kutoka Azam FC

Mchezaji Kipre Herman Tchetche amerejea Oman ilikukamilisha uhamisho wa kuanza kuichezea klabu yake mpya, Al-Nahda Al-Buraimi kutoka Azam FC ya Tanzania.

img_20160804_105729
Kipre Herman Tchetche alipo jiunga na klabu yake mpya, Al-Nahda Al-Buraimi

Tchetche alilazimika kurejea kwao, Ivory Coast mapema mwezi huu baada ya Azam FC kugoma kumruhusu kujiunga na Al Nahda bila dola za Kimarekani 50,000.

Na Azam ilifanya hivyo kwa sababu Tchetche aliondoka Dar es Salaam akiwa amebakiza Mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuichezea klabu hiyo tangu mwaka 2010.

Akizungumza na binzubeiry Tchetche amesema anatarajia kumalizana na Azam FC ndani ya muda mfupi tangu sasa. “Tayari nimerudi Oman na ninatarajia kumalizana na Azam muda si mrefu ili nianze kucheza hapa,” alisema Tchetche.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents