Michezo

Kipa wa Uganda Cranes aingia 10 bora ya makipa duniani

Mlinda mlango wa timu ya Taifa ya Uganda, Denis Masinde Onyango amewekwa kwenye 10 bora ya walinda mlango wa mwaka 2016.

Mlinda mlango huyo ambaye kwa sasa anadakia klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, anakamata nafasi ya 10, akiwa na pointi 5 baada ya kuchaguliwa na shirikisho la kimataifa la historia na takwimu ya mpira wa miguu (IFFHS).

Onyango alitwaa ubingwa wa Afrika na ligi kuu ya soka Afrika Kusini akiwa na Mamelod, huku pia akiwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayesakata kabumbu, ndani ya Afrika.

Onyango amewapita makipa bora kabisa Duniani, Petr Cech wa Arsenal na Marc Andre Ter Stegen wa Barcelona wanaoshika nafasi ya 11 na 13.

Nafasi ya kwanza ya mlinda mlango bora duniani kwa sasa inaendelea kushikiliwa na mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich Manuel Neuer.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents