Burudani

Kiongozi wa bendi ya rock, U2 na mwanzilishi wa One Campaign, Bono, kukutana na Kikwete na AY nchini

Kiongozi wa bendi maarufu duniani ya muziki wa rock, U2 ya nchini Ireland na mwanzilishi wa miradi mbalimbali barani Afrika ikiwemo One Campaign, DATA, EDUN na Product Red, Paul David Hewson maarufu kama Bono anatarajia kuja nchini Tanzania kufanya mazungumzo na Rais Jakaya Kikwete pamoja na AY.

Bono_at_the_2009_Tribeca_Film_Festival
Bono

“Ntakuwa na ugeni naye (Bono) wiki ijayo anakuja kukutana na president hapa kwahiyo amenitaarifu kwamba wiki ijayo itabidi tufanye meeting mimi na yeye,” AY ambaye ni miongoni mwa mabalozi wa Afrika wa kampeni ya One, ameiambia Nuru FM ya Iringa leo (20/8).

AY amesema madhumuni ya ziara ya Bono nchini ni kuangalia uwezekano wa kuweka kwenye kilimo nchini.

Bono ambaye ana utajiri ufikao dola milioni 600, anafahamika kwa shughuli zake za kibinadamu na kutoa misaada barani Africa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents