Habari

Kingunge: Mko wapi Marais wastaafu?

Aliyekuwa kada wa CCM na mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale Mwiru amewaomba Marais wastaafu kuzungumza na Rais Dkt John Magufuli ili asitishe maandamano yaliyopangwa kufanywa kufanyika September mosi mwaka huu.

_MG_6474

Akiongea na waandishi wa habari, Kingunge amewalaumu viongozi wastaafu wakiwemo marais pamoja na mawaziri wakuu kwa kukaa kimya wakati huu ambao nchi inatikiswa huku katiba ya Jamhuri ikisiginwa.

Marais-Wastaafu (1)
Picha ya Maraisi wastaafu

Miongoni mwa viongozi wanaolalamikiwa kutosikika ama kuchukua hatua zozote ili kuilinda Katiba ni pamoja na Marais Wastaafu, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Aman Abeid Karume (Zanzibar).

“Naomba Rais Magufuli, akubali kuitisha kikao na Chadema ambacho pia wazee wastaafu watahudhuria, akifanya hivyo hata sisi wazee tutawageukia Chadema na kuwaambia wasitishe mpango wao wa maandamano,” amesema Kingunge.

Hali hiyo imeibua mtikisiko mkubwa nchini huku viongozi wa dini, wanasiasa, wasomi na wananchi wa kawaida wakitaka kupatikana suluhu kabla ya Septemba Mosi, tarehe iliyopangwa kuanza maandamano na mikutano hiyo.

Kingunge ambaye alihamia Chadema akitokea CCM kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana kutokana na kutoridhishwa na namna mchakato wa kumpata mgombea urais kutoka chama hicho amesema, Chadema inatumia haki yake ya kikatiba.

CHANZO: MWANAHALISI

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents