Burudani

Kinachozikwamisha filamu za Kibongo movie ukosefu wa promotion

Ni lini mara ya mwisho umekutana na trailer ya filamu ya Kibongo mtandaoni au kwenye TV na ikakuvutia kiasi cha kuingia mtaani kuitafuta?

ukurasa_mpya

Lakini ni mara ngapi unaona trailer za filamu za Hollywood kwenye Youtube na kupata hamu kubwa ya kwenda kuiona kwenye majumba ya sinema kuiangalia ama kuzama kwenye torrent kuishusha? Naamini ni mara nyingi.

Biashara yoyote inahitaji matangazo. Haiwezekani watu wakaota tu kuwa Irene Uwoya ametoa filamu na wakaenda kuitafuta kwenye maduka ya movie. Ni lazima waandalie kwa muda mrefu kuhusu ujio wa filamu fulani kwa njia nyingi za promotion.

Kuweka poster pekee kwenye Instagram haitoshi. Basi walau hata Facebook ambayo ninaamini ina watazamaji wengi zaidi wa filamu za kibongo ingeweza kutumiwa vyema, watu wengi wangechangamkia.

Tatizo kubwa kwenye filamu za kibongo ni promotion na naamini kama haya yakifanywa soko la filamu hizo linaweza kukua na kuwepo mijadala zaidi.

Kutengeneza Trailer za Kuvutia

Trailer ni kiini cha promotion za filamu kwasababu ndizo zinazompa mtazamaji picha ya fupi ya filamu hiyo itakavyokuwa. Na kwa Hollywood trailer hutoka mapema, hata miezi sita au mwaka wakati mwingine kabla filamu haijatoka. Mara nyingi trailer za filamu za Kibongo ambazo nyingi hazina mvuto, huwekwa mwanzoni mwa filamu fulani. Kwa wenzetu, trailer huoneshwa kwenye majumba ya sinema. Huoneshwa kwenye majumba hayo kabla ya filamu zingine kuoneshwa au kwenye screen za nje. Trailer yenye dakika mbili na nusu na iliyotayarishwa vizuri inaweza kuwa na ushawishi mkubwa.

Posters

Hapa kidogo wasanii wabongo wanajitahidi na mara nyingi tumekuwa tukiona posters kadhaa kwenye kuta au nguzo za mtaani. Wasanii inabidi waende mbali zaidi kwa kutengeneza poster za kuwekwa kwenye stand au banner na kuwekwa kwenye maeneo yanayotembelewa na watu wengi.

Television na Radio

Wasambazaji wa filamu za Hollywood hutumia takriban dola bilioni 4 kila mwaka kulipitia matangazo kwenye redio au TV za filamu zao. TV ni muhimu zaidi kwasababu ni chombo cha sauti na picha na inaweza kufikisha ujumbe haraka. Hapa ndipo watengenezaji wa filamu za Tanzania wameshindwa kupafanyia kazi.

Kama ambavyo wasanii wa muziki wamekuwa wakifanya media tour kupromote single zao, waigizaji wanatakiwa kufanya hivyo pia. Ni kwasababu media tour hazihitaji kulipiwa iwapo bajeti ya kulipia matangazo ya kawaida haipo. Malengo ya interview ni kuwapa watangazaji au waandishi mambo exclusive kuhusiana na filamu hiyo kutoka kwa mastaa walioigiza. Hii inatengeneza buzz na kuwashawishi watu kuinunua.

Behind the Scenes

Hii ni muhimu sana na Hollywood wanaitumia mno ambapo wahusika wa filamu huelezea utengenezaji wa filamu husika na kuoneshwa baadhi ya vipande vya video wakiwa location. Hizi hutengenezwa kama documentary ambayo inaweza kurushwa kwenye TV au kuwekwa Youtube.

Viral Marketing

Hii inahusisha usambazaji wa bure wa trailer kwa website za burudani. Kutumia mitandao ya kijamii zaidi na hata kulipia matangazo kwenye mitandao hiyo ambayo huwezesha watu wengi zaidi kuona.

Magazeti

Kuweka tangazo kwenye magazeti au majarida yanayosomwa ni muhimu sana pia.

Kutoa zawadi

Kutoa zawadi mbalimbali kama vile t-shirt au kofia zinazopromote filamu. Hakuna mtu asiyependa kupewa zawadi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents