Burudani

Kilimanjaro yakutana na waandishi wa habari kuelezea mchakato wa kura za KTMA 2014

Kampuni ya bia ya Tanzania inayotengeneza kinywaji cha Kilimanjaro leo imekutana na waandishi wa habari kuzungumzia mwenendo wa mchakato wa kuwapata washindi wa vipengele vya tuzo za Tanzania – Kilimanjaro Tanzania Music Awards (KTMA).

1

Baada ya wa Tanzania kupendekeza wasanii kwa mujibu wa vigezo vya BASATA na Academy kupigia kura wateule kwenye vipengele hivyo sasa watanzania wanapiga kura kukamilisha asilimia 70 za kura za wapenzi na mashabiki wa muziki nchini.

“Kama ilivyo kawaida na tulivoelezea awali asilimia 30 za kura zitatoka kwa majaji ambao wanatazamiwa kukaa wiki hii,” amesema meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe. “Mwaka huu majaji watakaa kujadili kila msanii katika kila kipengele kwa vigezo vya ziada kama watakavyopewa na BASATA,” ameongeza.

Majaji mwaka huu ni mjumuisho wa wasimamizi/waandaji na waongoza vipindi vya chati mbalimbali za redio pamoja na runinga, wataalam wa muziki pamoja na wadau wa muziki nchini. Majaji wanatazamiwa kuwa 15 ambapo 8 ni kutoka kwenye chati za muziki za redio na runinga, wawili ni wataalam wa muziki na wa 5 ni wadau wa muziki.

Vigezo vya majaji vitawekwa hadharani vitakapokuwa tayari kutoka BASATA.

Kavishe alisisitiza kwa wa Tanzania kuendelea kupiga kura hasa kwa siku hizi chache zilizobaki ili kuwapa ushindi wa uhakika wapenzi wao. Alisisitiza kwa wa Tanzania kupiga kura kwa usahihi hasa za SMS. ‘Andika code ya msanii unaemtaka bila kuongeza neno lolote na utume kwenda namba 15440 na ukumbuke kura ni moja tu kwa kila kipengele’.

Maelezo ya ziada juu ya upigaji kura yanapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro .

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents