Awards

Kilimanjaro Music Awards 2013 kuonyeshwa live mtandaoni

Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8.

Blog-PR-KTMA-Post

Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini.

Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application ya *LIVESTREAM* itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013/live na katika Blogs mbalimbali.

Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbi zitapatikana kupitia ukurasa wa Instagram wa Kilimanjaro Premium Lager ambao ni www.instagram.com/kili_lager
wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents