Burudani

Kilichojiri wiki hii kwenye Bongo Star Search 2012

Jana jioni Bongo5 ilitimba katika kiota cha Budget maeneo ya Kunduchi Bahari Beach kushuhudia yale yanayojiri katika shindano la kusaka vipaji vya muziki la Bongo Star Search na kupata updates za namna mambo yanavyokwenda.

Moja kati ya update hizo ni pamoja na kuwa kwa sasa washiriki wamebaki kumi na kwamba Jumapili wawili am mmoja atayaaga mashindano hayo. Hivyo bado wanawahamasisha wadau wa shindano hilo kuwapigia kura washiriki wanaowapenda.

Washiriki waliopo kwenye kinyang’anyiro hicho ni pamoja na ‘Rocha Rocha,’ ni Menyanah Atiki mwenye namba za ushiriki EBSS 04, Linias Mhaya EBSS 03, Norman Severino EBSS 05, pamoja na mwenye namba EBSS 01.

Wiki iliyopita mshiriki Godfrey Kato, aliponea kwenye tundu la sindano na kunusurika baada ya kupata kura nyingi za kubaki.

Ni lile Shindano la Bongo Stars Search linazidi kushika kasi kwa kile kipindi kigumu cha washiriki kitaendelea tena siku ya Jumapili, kwa washiriki wengine wawili miongoni mwa kumi kuaga shindano hilo.

Wiki iliyopita, ilishuhudiwa washiriki Vincent Mushi na Salma Mahini wakitoka miongoni mwa washiriki 12 waliofanikiwa kuingia mjengoni.Naye Jaji Mkuu wa BSS, Madam Ritha Paulsen, ameendelea kuwasisitiza mashabiki wapige kura kwa wingi kuwaokoa washiriki wanaowapenda.

Alisema kwamba bila kura yako mshiriki unayempenda atatoka, kwa sasa shindano hilo liko mikononi mwa mashabiki kwa kuchagua mshindi wanaomtaka.

Tazama baadhi ya picha za waliokuwepo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents