Awards

Kili Music Tour: AY, FA, Profesa J, Vanessa, Ben Pol, Weusi kushusha burudani Jumamosi hii*

Baada ya kuzunguka kaskazini, kusini, kanda ya ziwa, kanda ya kati na nyanda za juu kusini Jumamosi hii burudani ya Kili Music Tour inamalizikia Leaders Club jijini Dar es Salaam.

KTMA Winners Tour - PR Post - DAR

Wasanii watakaotumbuiza ni pamoja na Christian Bella, Khadija Kopa, Jambo Squad, Ben Pol, Profesa Jay, Rich Mavoko, Vanessa Mdee, Ommy Dimpoz, MwanaFA, Weusi na Mashujaa Band.

Msanii mwingine atakayeongezeka kwenye show ya Dar ni Ambwene Yessaya aka AY ambaye mara nyingi amekuwa akishare jukwaa na swahiba wake wa siku nyingi, Hamis Mwinjuma aka Mwana FA.

Akiongea na Kikwetu Blog hivi karibuni, AY alidai kuwa kushiriki kwenye Kili Music Tour mwaka huu ni kitu alichokifurahia. “Kusema ukweli jinsi wanavyotutreat sisi kila kitu kiko sawa kuanzia masuala ya malipo, masuala ya malazi, usafiri na vitu vingine vya kikazi,” amesema AY. “Na kizuri kabisa kuliko zote ni kuwa wanazingatia discipline,” aliongeza.

Kuhusu ngoma ya pamoja na Mwana FA, AY alisema baada ya kila mmoja kutoa ngoma yake, atatoa wimbo mpya mwezi huu wa August na kabla ya mwaka 2014 kuisha, wamepanga kutoa wimbo wa pamoja.

Kiingilio kwenye show ya Kili Music Tour, Leaders Club Dar ni buku tatu tu, usikose!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents