Awards

Kili Music Awards 2012 Semina elekezi ya wasanii

Waandaji wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards leo walifanya semina elekezi na wasanii mbali mbali, Meneja Chapa wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe, amesema tuzo hizo ni kwa ajili ya kukuza tasnia ya muziki wa Tanzania katika soko la ndani na nje, kwakuwa ndiyo mmoja kati ya bidhaa kubwa zinayouzika kwa wingi nje.

Kavishe amewataka wasanii waache kususia tuzo hizo kwakuwa kila mwaka wanasikiliza maoni yao ili kuboresha tuzo hizo na kuzifikisha katika ubora wa kimataifa.

Pia Kavishe amewataka wasanii ambao watafanikiwa kuingia kwenye tuzo yoyote nje ya nchi, wanapokwama katika usafiri waweze kujulishwa kwakuwa wapo tayari kushirikiana na yoyote ili kuweza kufanikisha kwa hilo kama ilivyokuwa kwa msanii Cpwaa.

Kavishe amesisitiza kwamba Kili Tanzania Music Awards kwa sasa zinachukua nafasi ya pili kwa ukubwa na gharama barani Afrika baada ya tuzo za Kora kutoka South Africa kutofanyika mwaka 2011.

Amewataka wasanii kuweza kufikiria mbele kimuziki, kwakuwa tuzo za mwaka huu wanahitaji ziwe za kitofauti zaidi, kama walivyoweza kuzibadili za miaka miwili iliyopita, kwa kuthamini wanamuziki wa ndani katika kutoa burudani siku ya tuzo.

Amesema tuzo hizo hazina upendeleo wowote, kwakuwa Academy inayochagua wasanii hao ina watu 50, tofauti na mwanzo kwakuwa ni vigumu mtu kuweza kuwashawishi wote.

Wasanii walipata fursa ya kutoa maoni yao juu ya tuzo hiyo, akiwemo Saidi Fella kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe.
Fella aliomba japo kupewa tuzo moja ya umenejaa kutokana na kwamba tangu alipokuwa akimdhamini msanii Juma Kasim Nature ‘Juma Nature’ na baadaye Wanaume Family, Chege na Temba, hadi sasa Dogo Aslay hamna hata msanii mmoja kati yao aliyefanikiwa kupata tuzo.

Pia msanii H.Baba naye alilalamikia tangu kipindi hicho, anatoka na nyimbo kama Mpenzi Bubu, Kula lazima kuoga hiyari na nyingine ambazo zilifanya vizuri lakini hakuwekwa kwenye kinyanganyiro hicho, mpaka hii leo.
Aliongeza kwa kusema Kili Tanzania Muzic Awards, miongoni mwa waasisi wake ni marehemu Dandu, ambapo zilikuwa zikiitwa Dandu Planet Africa lakini cha ajabu wameshindwa hata kumuenzi kwa lolote lile.

Mwanamuziki kutoka mashujaa Chalz Baba naye alitetea upande wake kama mwwanamuziki wa Dansi kwa kusema, wao ndiyo watumbuizaji wakubwa lakini chaajabu kwenye kinyanganyiro hicho haawakuwemo jambo ambalo linawashangaza.

Jose Mara kutoka Mapacha Watatu, yeye ametoa maoni kwamba tuzo za mtunzi bora zibaki kwa wanamuziki wakongwe kutoka katika bendi za zamani kama Kilimanjaro Bendi ‘Wananjenje’, Msondo Ngoma na Sikinde, kwakuwa wao ni mazao kutoka kwa wasanii hao ambao wana mchango mkubwa kwenye muziki huu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents