Kili Music Awards 2009 Nominations

Kili Music Awards 2009 Nominations
Mashindano ya Kili Music Award yameingia hatua ya mwisho baada ya
kutajwa majina yaliyopendekezwa kuwania tuzo hizo kwa mwaka huu. Katika
hatua hiyo, wasanii Judith Wambura ‘Lady Jay Dee’, Mwasiti Almas,
Khadij Shaaban ‘Keisha’ na Isha Ramadhani watachuana kuwania tuzo ya
mwimbaji bora wa kike

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam Meneja wa Bia ya Kilimanjaro ambayo ndiyo waandaaji wa tuzo hizo, Oscar Shelukindo alisema kuwa kamati ilikaa na kuangalia majina yote yaliyopendekezwa na hatimaye kupata yale yatakayowania tuzo hizo.

“Kamati ilikaa na kupitia majina yote yaliyopendekezwa na hatimaye kupata majina ambayo yatawania tuzo katika vipengele tofauti kulingana na sifa tulizozihitaji.” “TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro Premium Lager inayofuraha kuweka majina ya wasanii na watayarishaji wa muziki hadharani ili kutoa fursa kwa Watanzania kupiga kura ili tupate mshindi kwa mwaka 2009 wa Kili Music Award kama tulivyofanya kwa miaka kadhaa iliyopita.

”Alisema Shelukindo. Nafasi ya mwimbaji bora wa kiume itawaniwa na Matonya, Makamua, M.B Dogg, Hammer Q na Q Jay wakati albam bora ya taarabu itashirikisha V.I.P ya Jahazi, Why ya TOT, Mwanamke Hulka ya East African Melody, Mwanamke Mvuto ya New Zanzibar na Ya Mwenzenu Midomoni ya Jahazi.

Katika wimbo bora wa mwaka ni pamoja na Tabasamu wa Mr Bluu aliomshirikisha Steve, Anita wa Matonya, Dar Mpaka Moro wa TMK Family V.I.P na Nzela wa B Band wakati wimbo bora wa Afrika Mashariki zinazoshindanishwa ni Sweet Love wa Wahu (Kenya), Ti-chi Ken Raz (Kenya), Zuwena Wezzre (Uganda), Sirimba Ngoni Ft Lady Jay dee (Uganda), Salary Nameless (Kenya).

Kipengele cha mtayarishaji bora wa nyimbo wanaowania ni Ambros (Dunga), Lamar, Marco Chali, Hamie B na Man Walter huku mtayarishaji bora wa video itashindaniwa na Vissual Lab, Kallaghe Production, Maujanja Supplier, Empty Souls pamoja na Outcome Production.

Aidha, Shelukindo alisema, mashindano hayo yatashirikisha kazi za muziki za mwaka 2008 na hivyo kuwataka wasanii kuyatumia mashindano hayo kuongeza ubunifu na ujuzi pamoja na kujua sheria zinazolinda haki zao. Mashindano hayo yamepangwa kufanyika wiki ya kwanza ya Aprili na wananchi watapata fursa ya kupiga kura ya kuchagua mshindi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms), kuponi za magazetini na pia kupitia tovuti ya www.kilitimetz.com

Bofya hapa kupata list kamili ya walioteuliwa Kili Music Awards 2009

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents