Michezo

Kichuya huenda akatua klabu ya Chippa United ya Afrika Kusini

Mchezaji wa klabu ya Simba ambaye hadi saivi ameonyesha kiwango cha juu tangu asajiliwe na Simba winga Shiza Kichuya huenda akaihama timu hiyo na kutua Chippa United ya Afrika Kusini baada ya benchi la ufundi la timu hiyo kuvutiwa naye.

shiza-kichuya-simba-2016_12v0abroioot81smmfxzi3nc9e

Wakala wa kusaka wachezaji wa timu ya Chippa, Rodgers Mathaba ameuambia mtandao wa Goal, kuwa wamevutiwa na mchezaji huyo baada ya kumfatilia katika baadhi ya mechi alizoichezea timu yake ya Simba na anatarajia kutua nchini hivi karibuni kwa ajili ya kufanya mazungumzo na uongozi wa timu hiyo.

“Tumevutiwa na kipaji cha Kichuya na tupo tayari kumnunua endapo tutafikia muafaka na klabu yake anayoichezea ya Simba,” amesema Mathaba.

Itakuwa ni neema kwa klabu ya Simba na Kichuya mwenye ambaye ametua Simba msimu huu akitokea Mtibwa Sugar na amekuwa na mwanzo mzuri hadi kufikia hapo alipo.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents