Michezo

Sam Allardyce apokonywa ukocha wa England

Kibarua cha kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Sam Allardyce kimeota mbawa kufuatia kauli yake kumponza wakati akiongea bila kujua na waandishi wa habari waliojifanya wafanyabiashara feki.

2d3e171500000578-0-image-a-8_1444493767563

Big Sam aliingia matatani baada ya kuwaeleza waandishi wa habari wa gazeti la Daily Telegraph waliojifanya wafanyabiashara kuwa ni rahisi kuizunguka sheria ya chama cha soka nchini Uingereza (FA) ya Mwaka 2008 ya kuzuia mchezaji kuwa mali ya mmiliki mwingine Kibiashara mbali ya Klabu yake.

Aidha taarifa iliyotolewa na gazeti hilo ilidai kuwa kocha huyo amemkashfu kocha wa timu hiyo ya taifa aliyepita [Roy Hodgson] na FA kwa kudai kuwa chama hicho kinajali fedha kuliko kitu kingine.

Sam Allardyce ameitumia timu hiyo kwa siku 67 tu na kucheza mechi moja peke yake.

Allardyce, 61, aliajiriwa July 22 na alikuwa na mkataba hadi mwaka 20018.

Tangazo la FA kumtimua katika kibarua hicho, limekuja saa 24 baada ya taarifa hizo za The Daily Telegraph kuandikwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents