Burudani

Khadija Kopa kuachia album mpya mbili, apanga kufanya kolabo na Diamond

Malkia wa Taarab, Khadija Khopa anatarajia kuachia album zake mbili ‘Lady with Confidence’ na ‘Kantangaze Akutangaze nani wakati hata mtaa wa pili hujulikani’.

SEMAGEN-SENDOFF-193-of-198

Akizungumza na Enewz ya EATV Khadija alisema anatarajia kuzizindua album hizo mpya mbili na pia anajiandaa kuizindua bendi yake maalum kwaajili ya watoto wake ambao nao watakuwa wakiimbia kwenye bendi hiyo.

Pia katika hatua nyingine Khadija, ameweka mipango yake wazi ya kufanya kazi na wasanii mbalimbali wa miondoko ya muziki wa Bongo flava wakiwemo Ommy Dimpoz, Diamond, Ali Kiba, Cassim Mganga, Chidi Benz na wengine baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan kuisha.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents