Habari

Kesi ya Kitilya na Shose Sinare (Miss Tanzania) yaahirishwa hadi Mei 3

Kesi ya aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake Sioi Solomoni na aliyekuwa afisa mwandamizi wa benki ya Stanibic tawi la Tanzania aliyekuwa mshindi wa taji la Miss Tanzania 1996, Shose Sinare. imehairishwa tena mpaka Mei 3.

13124954_1118898328174160_8279393462362525218_n

Leo April 29, kesi hiyo ilitajwa kusikilizwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam ambapo awali Hakimu Mchauru alitoa maamuzi ya kuahirishwa kwa kesi hiyo mpaka Mei 12 mwaka huu, sababu ni kutokana na jalada halisi la kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kukatwa kwa rufaa ya kufutiwa shitaka namba nane la utakatishaji fedha.

Muda mfupi baadaye majira ya saa 4;30 asubuhi walirudishwa tena mbele ya Hakimu Mchauru baada ya kupata amri kutoka kwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam akitamka kesi hiyo itajwe Mei 3 mwaka huu badala ya mei 12, aliyoipanga awali.

Hakimu Mchauru amesema sababu za kupewa amri hiyo hazijui, hivyo kesi itatajwa tena Mei 3 mwaka huu na yale yaliyozungumzwa asubuhi yatabaki kama ilivyo, watuhumiwa wote wamerudishwa rumande.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents