Habari

‘Kerewa’ ya Shetta yaingia kwenye Top 10 za Radio 3 Nigeria, NAIJA 102.7 FM, CITY 105.1 FM na THE BEAT 99.9FM

Shetta ameanza kuona matunda ya video yake ya ‘Kerewa’ aliyoifanya Afrika Kusini na director GodFather. Baada ya video yake kuanza kuchezwa kwenye vituo vya kimataifa kama MTV Base, Channel O na Soundcity, wimbo huo aliomshirikisha Diamond Platnumz umeingia kwenye Top 10 za Radio tatu za Nigeria.

shettaa

Kupitia chati ya NAIJA 102.7 FM ‘Kerewa’ ipo nafasi ya 4, kwenye chati ya CITY 105.1 FM ipo kwenye nafasi ya 9, na katika chati ya THE BEAT 99.9 FM Ijumaa iliyopita ilikamata nafasi ya 4. Radio zote tatu ni za Lagos, Nigeria.
NAIJA FM
Naija 102.7 FM (August 16) walitweet:

“#Naijafm #AfricanTop10 W @jollyswit #Np-no4,Kerewa @ShettaTz @diamondplatnumz (Tan).”

Shetta aliandika Instagram:

“Ukiwa unapiga kazi na unaona vitu kama hivi vinatokea kiukwel inatia moyo na kusema acha tuendelee kukomaa na kitaeleweka tu siku 1… Hii hapo ni #Kerewa ikionekana kuendelea kufanya vizuri kwenye chat mbalimbali za tv na radio tofauti kwenye mataifa mengine, hapo ikiwa imeshika #4 kwenye kituo cha radio huko Nigeria kinachoitwa #Naijafm102.7 #Africantop10… Big S/o to #Naijafm102.7Nigeria #striveforgreatness #Tanzania“

Cityfm

City 105 FM (August 17) nao walitweet:

“#NP 9. @ShettaTz ft @diamondplatnumz – Kerewa on African Music Chart @elishabaza Show”

Shetta alishare Instagram na kuandika:

“Hakika mziki wetu unakubalika na kukua kwa kasi sanaaaaa Hizi ni juhudi zetu sisi wenyewe But tunahitaji support kubwa kutoka nyumbani ili tuzidi kuendelea mbelee… Hii nyingine kutoka Nigeria #Africanmusicchat #Kerewa #No9 Big S/o #Cityfm105.1”

Beat-FM

THE BEAT 99.9 FM (August 15) walitweet:

Wasanii wengine wa Afrika Mashariki walioko kwenye chati ya NAIJA 102.7 FM ni pamoja na Radio na Weasel ‘Breath Away’ (Uganda) namba 2, na AY ‘Asante’ (Tanzania) nafasi ya 5.

Wasanii wengine walioko kwenye chati ya CITY 105.1 FM ni pamoja na Sauti Sol ‘Nishike Mkono’ (Kenya) kwenye nafasi ya 3, Mafikizolo ft. Davido ‘Tchelete’ (South Africa) namba 4, Radio na Weasel ‘Breath Away’ (Uganda) namba 5. Wengine ni Elani ‘Barua Ya Dunia’ (Kenya), Wimbo ulioshika nafasi ya kwanza kwenye chati hiyo ni DBlack GH ft.Castro Destroyer ‘Personal Person.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents