Burudani

Keisha adai muziki mgumu, azungumzia maisha ya muziki akiwa mama wa watoto 2

Msanii wa muziki ambaYe pia ni mama wa watoto wawili, Khadija Shaaban maarufu kama ‘Keisha amesema amejipanga kikamilifu kapambana na soko la muziki ambalo amedai kuwa ni gumu sana kwa sasa.

keisha

Akizungumza na Bongo5 leo, Keisha amesema kuwa muziki wa sasa hivi unahitaji uwekeze pesa nyingi ndipo ukulipe.

“Soko la muziki ni gumu kwa sababu tayari kuna watu wameshaweka pesa mbele kwenye muziki, kwahiyo ni lazima mtu ukae na ujipange, kwamba mtu anaweza akaenda radio na akatoa milioni kumi ya promotion halafu unategemea wewe uende radio na maneno matupu? Hawatapiga nyimbo yako, sio rahisi. Kwahiyo soko gumu kiukweli, muziki umekuwa biashara ‘nipe nikupe’,” amesema Keisha

Katika hatua nyingine Keisha amezungumzia ujio wake ingawa amedai familia nayo inataji muda wake zaidi.

“Sasa nataka niangalie watu wamemisi nini kutoka kwa Keisha, yupi? kwakuwa kuna Keisha wengi. Kuna Keisha wa ‘Uvumilivu’, kuna Keisha wa ‘Nimechoka’, na nyimbo zote na namna hiyo ninazo, kwaHiyo sijajua ni ipi mashabiki wangu wataipenda. Kwasababu solution sio kuhonga, kama unahonga lazima uwe na kitu kizuri maanake unaweza ukahonga kwenye kitu kibaya na usifanye vizuri. Kwahiyo nina nyimbo za aina nyingi tu sema naangalia ni nyimbo ipi Watanzania wataipenda au ni Keisha yupi watu wanamwitaji. Familia nayo ipo siwezi kuwa kama Keisha yule wa zamani au ambaye alikuwa na mtoto mmoja ingawa yule yupo shule na mwingine huyu mdogo kwahiyo wanahitaji malezi yangu zaidi na vitu vingi lakini kizuri zaidi tayari nilishafanya nyimbo, tayari ninazo kwahiyo nilijipanga nikarekodi wakati nina muda. Sasa hivi watu wasubiri mambo mazuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents