Burudani

Kassim Mganga kuachia albamu yake mpya yenye nyimbo 15

Msanii wa muziki mwenye nyimbo za kubembeleza, Kassim Mganga amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa mkao wa kula kwajili ya ujio wa albamu yake mpya ambayo itakuwa na nyimbo 15.

Muimbaji huyo aliachia albamu yake ya mwisho mwaka 2008 iitwayo ‘Haiwezekani’ na kufanya vizuri.

Alhamisi hii muimbaji huyo alipost picha ya cover la albamu yake iliyopita na kuweka wazi kuhusu ujio wa albamu hiyo mpya.

“Tbt 2008 -9 year back, #HaiwezekaniAlbum /pana haja ya kufanya tukio kubwa la kihistoria la hii safari ya muziki mtamu wa Tajiri,” aliandika Kassim Instagram.

Aliongeza, “Lakini kati ya moja kubwa kwenu mashabiki wangu ni kujiandaa tena kwa kuipokea albamu yangu mpya yenye takribani nyimbo 15 ndani ya mwaka huu,”

Muimbaji huyo amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia wimbo mpya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents