Burudani

Kanye West atoswa kuitwa kutumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Trump

Kanye West kapigwa mikausho mikali licha ya kuwa na matarajio kuwa angekuwa mmoja wa wasanii ambao wangetumbuiza kwenye sherehe za kuapishwa kwa Donald Trump, Ijumaa hii.

Jumatano hii mwenyekiti wa kamati ya sherehe hizo, Tom Barrack Jr.,alidai kuwa Yeezy hatotumbuiza. Aliiambia CNN kuwa licha ya Kanye kuwa mtu mzuri, hilo si jukwaa la muziki wa aina yake.

“We haven’t asked him. I mean, he’s been great. He considers himself a friend of the president-elect, but it’s not the venue. The venue we have for entertainment is filled out. It’s perfect. It’s going to be typically and traditionally American. Kanye’s a great guy. We just haven’t asked him to perform. We move on with our agenda,” alisema.

Wengi wamemkosoa Barrack kwa kauli yake kuwa Kanye hakuwa na vigezo vya kuwa Mmarekani asili na kudai kuwa ni maneno ya kibaguzi wa rangi. Kanye West amekuwa akikoselewa vikali kwa kumuunga mkono Trump ambapo rapper T.I. amemuita msaliti.

Sherehe hizo za kuapishwa kwa Trump zimesababisha mgawanyiko mkubwa ambapo muimbaji Chrisette Michele amekosolewa vikali kwa kutangaza kuwa atatumbuiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents