Burudani

Kanye West aonekana kwa mara ya kwanza tangu atoke hospitali

Baada ya takriban wiki mbili kutokuwa machoni mwa watu, Kanye West ameonekana kwa mara ya kwanza.

1208-kanye-west-blonde-instagram-5

Ameonekana Alhamis hii jijini Los Angeles katika eneo ambalo hutengeneza vitu mbalimbali vya sanaa, Pacific Design Center. Katika picha iliyowekwa kwenye mtandao wa TMZ, Kanye anaonekana akiwa amezipaka rangi (blonde) nywele zake.

Rapper huyo alikuwa amelazwa kwa siku 10 hospitali kufuatia uchovu wa kiakili na kuruhusiwa kwenda kuendelea na matibabu nyumbani. Tayari imedaiwa kuwa ameanza kuandaa album yake mpya kupitia studio yake ya nyumbani.

Wakati huo huo, rafiki wa karibu wa Kim Kardashian, amekanusha tetesi za mrembo huyo kutaka kuachana na Kanye West.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents