Burudani

Kanye West amchana Jay Z: Our kids ain’t never even played together’

Nilikuwa nategemea kuna siku kama hii itafika. Tangu Jay Z na Beyonce watose kuhudhuria harusi ya Kanye West na Kim Kardashian miaka miwili iliyopita, urafiki wa Yeezy na Hov uliingia matatani.

beyonce-featuring-jay-z-kanye-west-drunk-in-love-remix

Wawili hao kila mmoja amekuwa na maisha yake na kinachowaunganisha sasa ni mtandao wa Tidal wanaoumiliki pamoja, lakini hakuna urafiki tena.

Na sasa Kanye yamemfika shingoni na ameamua kuyatoa. Akiwa kwenye show ya ziara yake ya Saint Pablo huko Seattle, Yeezy amemchana Hov kwa masuala kibao, kikazi hadi kifamilia.

Amelalamika kuwa watoto wao, hata hawajahi kukutana na kucheza pamoja licha ya kile wanachokiamini kuwa ni marafiki. “I can’t take this shit, bro,” alisema katikati ya show hiyo.

“Our kids ain’t never even played together.”

Yeezy alimchana pia Jigga kuwa asimpigie simu kumpa pole kwa mkasa wa mkewe kuvamiwa na kuporwa huko Paris, bali anatakiwa kwenda nyumbani kwake na kumsalimia.

“You wanna know how I’m feeling?” Don’t call me, after the robbery, and say ‘how you feelin?’ You wanna know how I’m feelin? Come by the house. Bring the kids by the house like we brothers. Let’s sit down.”

Pia Kanye alizungumzia uadui wa Tidal na Apple unaomkera ambao anaamini unazuia mambo mengi, huku akimtupia lawama Jay Z kuwa chanzo. Alieleza pia kuwa mashabiki wasitarajie album nyingine ya Watch the Throne.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents