Burudani

Kanye na Kim watumia tshs mil 835 kupata mtoto anayefanana na North West ili kujihami na mapaparazi

Kanye and Kim West hawako tayari kuona maisha ya mtoto wao, North yanaingia hatarani. Kuhakikisha kuwa mtoto wao hawehuki kwasababu ya usumbufu wa mapaparazi, Kanye na Kim wametumia $500,000 (zaidi ya shilingi milioni 835) kupata mtoto anayefanana na wa kwao.

kanye-west-kim-kardashian-north-west-vogue-3
North West

Kwa mujibu wa gazeti la The Mirror, mastaa hao wametumia kiasi hicho kikubwa cha fedha kutafuta mtoto anayefanana vile vile na binti yao North. Kama hiyo haitoshi, wawili hao pia wametafuta mlezi wa mtoto anayefanana na mlezi halisi ili kuwachanganya kabisa mapaparazi.

Hata hivyo, Kanye na Kim sio wazazi wa kwanza kuwahi kufanya hivyo. Tom Cruise na Katie Holmes nao waliwahi kufanya hivyo kwa binti yao Suri wakati akiwa mdogo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents