Burudani

Kanye na Kim kulipwa $440,000 na mwanzilishi wa Youtube aliyevujisha video yao wakati wakivishana pete!

Mwanzilishi wa mtandao wa Youtube atalazimika kuwatajirisha zaidi Kim Kardashian na Kanye West baada ya kutakiwa kuwalipa $440,000 kutokana na kurekodi video kwa siri wakati wawili hao walipokuwa wakivishana pete na kuiweka mtandaoni.

Kim-Kardashian-and-Kanye-West-wedding

Mtandao wa TMZ umedai kuwa Chad Hurley amekubali kuwalipa wanandoa hao kwa kukiuka masharti.

Tukio hilo lilitokea mwaka 2013 ambapo Hurley alikuwa mmoja wa waalikwa na alisaini mkataba wa kutotoa siri. Hurley alirekodi video hiyo kwa siri na kuiweka kwenye mtandao wake wa MixBit.

Anatakiwa kulipa kiasi hicho cha fedha katika siku chache zijazo.

$400k si fedha nyingi kwa Hurley hasa ukizingatia kuwa aliiuza YouTube kwa dola bilioni 1.6.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents